Rais wa klabu ya PSG Nasser Al Khelafi amesema kua klabu hiyo ipo kwenye muenendo mzuri licha ya kuanza vibaya mashindano yao mbalimbali msimu huu.

Rais Nasser Al Khelaifi amesema wamefanya mabadiliko makubwa sana kipindi hichi kuliko wakati wowote klabuni hapo, Hivo wanajua wanahitajika kua wavumilivu kwakua wapo kwenye njia sahihi.nasser al khelaifiPSG wamefanya mabadiliko mbalimbali kuanzia kwenye uongozi mpaka kwa wachezaji ambapo walimtoa kocha aliyekuepo msimu uliomalizika Christopher Galtier na kumleta Luis Enrique, Lakini pia wakiondoa baadhi ya wachezaji muhimu klabuni hapo kama Lionel Messi na Neymar Jr.

Rais wa klabu hiyo Nasser Al Khelaifi anaamini mabadiliko ambayo wameyafanya klabuni hapo yataleta matunda siku za mbeleni, Kwani anaamini wamefanya mamuzi sahihi na yatawalipa siku za usoni.nasser al khelaifiKlabu ya PSG imekua na mwanzo mbaya kwenye ligi ya Ufaransa jambo ambalo sio la kawaida kitu ambacho kimefanya mashabiki kuanza kuwaekea mashaka, Lakini Rais wa klabu hiyo anaamini wanahitaji uvumilivu ili mabadiliko waliyoyafanya yaanze kuleta matunda.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa