Nketiah Kutimkia Marseille

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Eddie Nketiah anatajwa yuko mbioni kujiunga na klabu ya Olympique Marseille kuelekea msimu ujao wa 2024/25.

Eddie Nketiah amekua sio chaguo la kwanza ndani ya klabu ya Arsenal kwa muda mrefu tangu apande kutoka timu ya vijana ya klabu hiyo miaka kadhaa nyuma, Hivo imemfanya mshambuliaji huyo kuamua kutafuta changamoto nyingine kuelekea msimu ujao na Olympique Marseille ndio imekua chaguo lake.nketiahMshambuliaji huyo inaelezwa amefikia makubaliano na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, Hivo kinachosubiriwa ni klabu ya  Marseille kutoa kiwango cha pesa amcaho kitakubaliwa na klabu ya Arsenal ili mshambuliaji huyo aweze kujiunga na klabu hiyo.

Mazungumzo yanaendelea baina ya vilabu hivo viwili ili kuhakikisha dili hilo linakamilika haraka iwezekanavyo kwani klabu ya Arsenal wenyewe wako tayari kumuuza mchezaji huyo, Mshambuliaji Nketiah akikamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Marseille ataungana na Mason Greenwood mshambuliaji wa zamani wa Man United.

Acha ujumbe