Nuno Mendes Ajifunga PSG

Beki wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ureno Nuno Mendes anaelezwa yuko mbioni kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo mabingwa watetezi wa Ufaransa mpaka mwaka 2029.

Klabu ya PSG ipo kwenye mchakato wa kutengeneza mradi wa muda mrefu klabu hapo na ndio maana wanawaongezea mkataba wachezaji wake muhimu haswa wenye umri mdogo, Ukiachana na Nuno Mendes ambaye siku yeyote atatangazwa kuongeza mkataba lakini pia wamemuongeza Achraf Hakimi.nuno mendesMabingwa hao wa Ufaransa chini ya kocha Luis Enrique wana mpango wa kuhakikisha wanafanya vizuri sana haswa kwenye ligi ya mabingwa ulaya na ndio sababu ya kuisuka timu hiyo kwa kusajili vijana wadogo wenye vipaji vikubwa, Lakini pia kuwaongezea mikataba wachezaji wenye ubora kikosini.

Nuno Mendes amekua kwenye kiwango bora sana tangu atue ndani ya kikosi cha PSG na kufanikiwa kua mchezaji muhimu ndani ya klabu hiyo licha ya kuandamwa na majeraha msimu wa 2022/23, Lakini msimu uliomalizika na msimu ameendelea kuonesha ubora mkubwa sana na kuwafanya mabosi wa klabu hiyo kuendelea kuhitaji huduma yake ndani ya viunga vya Parc de Princes.

Acha ujumbe