Klabu ya Olympique Lyon imemtimua kocha wake Fabio Grosso baada ya matokeo mabaya ambayo yanaendelea kutokea ndani ya klabu hiyo kwenye michuano mbalimbali.
Klabu ya Olympique lyon imefukuza makocha takribani baada ya msimu huu kuanza na yote ni kutokana na matokeo yasiyo ya kuridhisha ambayo klabu hiyo inaendelea kuyapata.Klabu hiyo imetangaza kuachana na Fabio Grosso leo tarehe 30 Novemba lakini mwezi Septemba mwaka huu klabu hiyo iliachana na aliyekua kocha wake Laurent Blanc raia wa kimataifa wa Ufaransa kutokana na matokeo mabaya pia.
Klabu hiyo ipo mkiani kabisa mwa msimamo wa ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 wakiwa na alama 7 tu baada ya kucheza michezo 12 kwenye ligi hiyo, Jambo ambalo ni geni kwa klabu hiyo ambayo imewahi kushinda taji la ligi hiyo mara saba mfululizo.Baada ya kuachana na Fabio Grosso klabu ya Olympique Lyon imemteua Pierre Sage kama kocha wa muda, Huku viongozi wa klabu hiyo wakiwa wanashughulikia kutafuta kocha mpya wa kudumu ambaye atairudisha klabu hiyo kwenye ubora.