Klabu ya PSG iko mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa klabu ya Benfica na timu ya tifa ya Ureno Goncalo Ramos ambaye inaelezwa ameshamlizana na mabingwa hao wa Ufaransa.
Klabu ya PSG inatarajiwa kutuma ofa ya Euro milioni 80 ambayo itajumuisha bonasi huku mchezaji Goncalo Ramos akielezwa kukubali mkataba wa miaka mitano mpaka mwaka 2028.Kocha mpya wa mabingwa hao wa Ufaransa Luis Enrique mpaka sasa anaonekana kufanya sajili zenye tija ndani ya klabu hiyo, Huku wengi wakianza kuitabiria makubwa klabu hiyo kuelekea msimu ujao haswa kwenye michuano ya ulaya.
Goncalo Ramos ni miongoni mwa washambuliaji waliokuepo kwenye orodha ya klabu ya Manchester United, Lakini alikua chaguo la pili endapo tu klabu hiyo ingemkosa mshambuliaji Rasmus Hojlund ambaye wameshampata kwasasa.Klabu ya PSG imebakiza baadhi ya vitu vichache sana kukamilisha usajili wa mshambuliaji Goncalo Ramos na mpaka sasa dili lilipofikia ni wazi haliwezi kuvunjika, Hivo wakati wowote kuanzia sasa mshambuliaji huyo atatangazwa kuhamia klabu hiyo mabingwa wa soka nchini Ufaransa.