PSG kwa Joao Neves ni Suala la Muda Tu

Mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa klabu ya PSG imefika hatua nzuri katika kuhakikisha wanapata saini ya kiungo wa klabu ya Benfica raia wa kimatiafa wa Ureno Joao Neves.

PSG wanaelezwa kumalizana katika maslahi binafsi  na Joao Neves wakati ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na klabu ya Benfica ili kuhakikisha wanakamilisha dili hilo, Kwani mpaka sasa sehemu pekee ambayo imebaki ili kufanya dili hilo likamilike ni makubaliano ya vilabu hivyo viwili.PSGKiungo Joao Neves amekua kwenye kiwango kikubwa ndani ya klabu ya Benfica mpaka kufikia kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kilichoshiriki michuano ya Euro 2024 licha ya umri wake kua mdogo, Jmabo ambalo limewavutia zaidi mabingwa hao wa soka kutoka nchini Ufaransa.

Klabu ya PSG ipo kwenye hatua nzuri ya kukamilisha dili la kumchukua Joao Neves kwakua mazungumzo yao baina ya klabu ya Benfica yanaelezwa kufikia hatua nzuri, Hivo ni wazi kiungo Joao Neves kutua ndani ya viunga vya Parc de Princes ni suala la muda kutokana na hatua waliyofikia vilabu hivo na mchezaji mwenyewe kukubali kujiunga na PSG.

Makala iliyopita

Acha ujumbe