Klabu ya PSG inaelezwa ina mipango mikubwa na kiungo wake fundi raia wa kimataifa wa Uholanzi Xavi Simons ambaye anakipiga katika klabu ya Rb Leipzig kwasasa kwa mkopo.
PSG wanaelezwa wana mpango mkubwa na kiungo huyo na kutaka kumfanya kama sura ya mradi wao wa siku za mbeleni, Hivo klabu hiyo ipo kwenye mchakato wa kumuongezea mkataba wa muda mrefu zaidi ndani ya timu hiyo.Klabu hiyo inafikiria kua na mradi mpya wa timu ambao utaundwa na vijana wadogo wenye ubora mkubwa, Huku Xavi Simons akiwa ndio kipaumbele cha klabu hiyo akiwa na kijana mwingine mdogo Warren Zaire Emery.
Kiungo Warren Zaire Emery inaelezwa ameshamalizana na klabu hiyo katika dili la kusaini mkataba mpya, Hivo hii inakupa picha kabisa namna gani klabu hiyo inapanga kusuka timu yenye ubora kupitia vijana wadogo na vipaumbele vimekua kwa Xavi Simons na Warren Zaire Emery.Kiungo Xavi Simons anapangwa kua sura ya mradi mpya klabuni hapo na hii ikielezwa ni kutokana na kuondoka kwa Kylian Mbappendani ya PSG mwishoni mwa msimu huu, Hivo kiungo huyo wa kidachi ndio anapewa kipaumbele sana akiwa anafanya vizuri sana kwasasa akiwa kwa mkopo klabu ya Rb Leipzig.