Klabu ya PSG imetuma ofa ya Euro milioni 50 kwa klabu ya Atalanta ya nchini Italia kwajili ya kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Rasmus Hojlund.

Klabu ya PSG imekua ikifukuzia saini ya mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Denmark kwa muda sasa, Hivo leo wametuma ofa rasmi kwa kijana huyo kwajili ya kuhakikisha anatua katika viunga vya Parc de Princes.PSGMabingwa wa Ufaransa wanahitaji mshambuliaji katika klabu hiyo baada ya kmruhusu mshambuliaji wao raia wa kimataifa wa Argentina ambaye ametimkia nchini Uturuki katika klabu ya Galatasaray mabingwa wa nchi hiyo.

PSG chini ya kocha Luis Enrique wanataka kutengeneza timu mpya ya ushindani na mshambuliaji Hojlund anaonekana kama mtu sahihi wa kuongoza safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo kipindi hichi ambacho Mbappe amewekwa sokoni.PSGMabingwa hao wa Ufaransa wako kwenye upinzani mkali kwani Man United nao wanamuhitaji mshambuliaji huyo kwa namna yeyote ambapo wao jana walituma kiasi cha Euro milioni 60, Huku Atalanta wakiwa wanataka Euro milioni 70 hivo vilabu vyote vinatakiwa kuongeza hela ili kumpata mchezaji huyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa