PSG Wana Matumaini ya Kumuongezea Messi Mkataba

Rais wa klabu ya PSG Nasser Al-Khelaifi amesema ana matumaini kua staa wa timu hiyo Lionel Messi ataongeza mkataba wa kusalia ndani ya viunga vya Parc de Princes.

Mchezaji huyo ambaye alisaini mkataba wa miaka mwili ndani ya miamba hiyo ya soka nchini Ufaransa lakini hivo mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Kuna taarifa zinaeleza wakati michuano ya kombe la dunia ianendelea staa huyo ameshakubaliana na klabu ya Inter Miami inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani maarufu kama MLS.psgTaarifa za watu wa karibu kutoka kwa mchezaji huyo pia zinaeleza kua Lionel Messi hana mpango wa kufanya maamuzi yeyote kuhusu hatma yake ndani ya PSG mpaka michuano ya kombe la dunia itakapomalizika mwezi huu.

Al-Khelaifi anaamini Messi ataongeza mkataba ndani ya timu hiyo kwasababu ana furaha klabuni hapo huku akisema kama mchezaji hana furaha kwenye timu hawezi kuonesha ubora mkubwa lakini mchezaji huyo msimu huu amekua kwenye kiwango bora sana.psgKumekua na taarifa mbalimbali kumhusu nahodha huyo wa timu ya taifa ya Argentina huku nyingi zikimhusisha kutimkia nchini Marekani lakini rais Khelaifi kutoka PSG yeye anaamini staa huyo atamwaga wino kuendelea kusalia kwenye viunga vya Parc de Princes.

Acha ujumbe