PSG Yathibitisha Kutemana na Tuchel.

Hatimaye uongozi wa PSG umethibitisha kukatisha mkataba na aliyekuwa kocha wa timu hiyo – Thomas Tuchel.

Tuchel alisimamishwa kazi siku ya mkesha wa Krismasi ikiwa ni miezi 4 tu tangu aiongoze timu hiyo kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Hapakuwa na taarifa rasmi kutoka PSG kuhusu tukio hilo ambalo linahusishwa na Mauricio Pochettino kujiunga na miamba hiyo ya soka la Ufaransa – Ligue 1.

Leo, raisi wa PSG –  Nasser Al-Khelaifi amethibitisha hilo. Nasser amesema “Nina mshukuru Thomas Tuchel na benchi lake la ufundi kwa aliyoyafanikisha kwenye klabu yetu.

Nasser Al- Khelaifi (kushoto) akiwa na Thomas Tuchel (kulia).

Thomas aliweka nguvu kubwa kwenye kazi yake na tutamkumbuka kwa nyakati zote tulizokuwa pamoja. Tunamtakia kila la kheri katika kazi yake.”

Taarifa ya kuthibitisho zimechelewa kutokana na taratibu za kisheria hasa fidia ambayo Tuchel anapaswa kulipwa, kocha huyo atapokea takribani pauni milioni 5 kama sehemu ya fidia yake.

Huwenda Pochettino atatangazwa kama kocha mpya wa klabu hiyo baada ya kuwa nje ya benchi la ufundi tangu Septemba 2019.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

18 Komentara

    Kila la kheri

    Jibu

    Huenda tukamuona Tuchel Uingereza ndani ya EPL

    Jibu

    Pole Tuchel

    Jibu

    Mmh psg inasua msimu huu

    Jibu

    Tuchel pole

    Jibu

    Mhh ata sijui cha kuandika

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Kweli vilabu vingi vya soka havitaki masihara ukizingua wanakutema

    Jibu

    Kwaheri kocha

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Nilikuwa namkubali sana Tuchel

    Jibu

    Popote kambi

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Kambi popote

    Jibu

    Kocha usikate Tamaa maisha popote

    Jibu

Acha ujumbe