PSG Yakaribia Kumnasa Enrique

Klabu ya PSG ipo mbioni kumalizana na aliyekua kocha wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique kama kocha wao mkuu kwa msimu ujao.

Klabu ya PSG imefikia hatua nzuri katika mazungumzo baina yao na kocha Enrique ili kuweza kumsaini kocha huyo aiongoze timu hiyo kuanzia msimu ujao baada ya kocha wa zamani wa Bayern Munich Julian Nagelsman kuikataa timu hiyo.PSGMabingwa hao wa Ufaransa wanahaha kupata kocha mwenye ubora sokoni kwasasa kwani tayari wameshafanya mazungumzo na makocha kadhaa mpaka sasa kabla ya Enrique, Lakini bado hawajafanikiwa kumpata kocha mkuu wa timu hiyo msimu ujao.

Klabu ya PSG imekua ina uchu mkubwa wa kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya kutokana na uwekezaji ambao wamekua wakiufanya ndani ya klabu hiyo, Huku makocha wengi wakiondolewa hapo kutokana na kushndwa kufikia malengo hayo.PSGPSG imekua ikifukuza makocha mara kwa mara kwasababu ya kushindwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa, Lakini Enrique kama atafanikiwa kupewa timu hiyo anaweza kuwafikisha nchi ya ahadi kwani kocha huyo ana uzoefu wa michuano hiyo kwani tayari ameshawahi kutwaa taji hilo na Barcelona.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.