Rais wa klabu PSG Naseer Al Khelaaf amekanusha kuhusiana na klabu hiyo kutaka kumsajili mchezaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United,Juventus, pamoja na klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Cristiano Ronaldo ambaye alikua mchezaji wa klabu wa Manchester United miezi kadhaa iliyopita lakini alitangaza kuachana na klabu hiyo huku kwasasa akiwa anahusishwa na timu mbalimbali barani ulaya na nchi za Urabuni.Mchezaji huyo ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kwasasa kama nahodha wa timu hiyo anatarajiwa kujiunga na klabu ambayo itafikia makubaliano na mchezaji huyo punde tu baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika nchini Qatar.
Rais Naseer Al Khelaaf pale alipoulizwa na wanahabari juu ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ureno na kusema “Kumsajili Ronaldo? Tuna wachezaji watatu Messi.Mbappe na Neymar ni ngumu kufikiri kuhusu Ronaldo. Namtakia kila la kheiri kwasababu bado ni mchezaji bora na mzuri sana”Ikumbukwe wiki kadhaa nyuma Rais huyo wa PSG aliweka wazi kua klabu hiyo haina mpango wa kuingia sokoni kwenye dirisha dogo la mwezi Januari, Kwababu timu yao ina wachezaji wazuri na haina ulazima wa kuingia sokoni.