Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid Sergio Ramos ambaye anakipiga klabu ya PSG kwasasa ametangaza kustaafu timu ya taifa ya Hispania ambayo ameitumikia kwa muda mrefu.
Sergio Ramos ametangaza kuachana na Hispania jioni ya leo baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa, Kupitia kurasa zake za mitandano yake ya kijamii gwiji huyo ametangaza kuachana na timu ya taifa ya nchi hiyo huku akiandika ujumbe mrefu ambao umeacha maswali mengi.Nahodha huyo wa zamani wa Hispania ambaye ameshinda taji la Euro 2008 na 2012 pamoja na kombe la dunia mwaka 2010 ameamua kuachana na timu hiyo kutokana na sababu ambazo amezieleza huku umri ukiwa sio sababu, Beki huyo ameeleza kua mwalimu wasasa wa timu hiyo amempigia simu na kumueleza kua hayupo kwenye mipango yake ya sasa na hata ya baadae na haitajalisha uwezo ambao anauonesha.
Kupitia ujumbe ambao Ramos ameandika kuachana na timu ya taifa ya Hispania kua mahali ameandika kua mpira hauna usawa kila siku na vilevile mpira haujawahi kua mpira tu, Kutokana na kauli hii inaonesha wazi kua beki huyo kuna mambo mengi ambayo yamemsukuma kuachana na timu hiyo.Sergio Ramos pamoja na kuachana na timu ya taifa Hispania lakini atakumbukwa kama moja ya mchezaji bora kuwahi kutokea katika timu hiyo, Vilevile kama mchezaji aliyepata mafanikio makubwa zaidi ndani ya timu hiyo kwani beki huyo amefanikiwa kushinda kila taji kubwa na timu ya taifa ya Hispania ikiwemo mataifa ya ulaya maarufu kama Euro akitwaa mara mbili na kombe la dunia mwaka 2010.