Simeone: Mimi ndo Naangusha wachezaji wangu

Kocha wa klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amesema inawezekana kwasasa yeye ndo anaiangusha klabu hiyo pamoja na wachezaji wake.

Klabu ya Atletico Madrid ambayo imeshinda ubingwa wa La liga msimu wa 2020/21, Lakini mpaka sasa wanaonekana hawapo kwenye mbio za ubingwa kwani mpaka sasa wapo kwenye nafasi ya tano wakiwa na alama 24 huku vinara Barca wakiwa na alama 37.simeoneKocha Diego Simeone anaamini kua klabu hiyo bado ina uwezo wa kupambana kugombania taji la ligi kuu ya Uingereza, Huku akisema inawezekana yeye ndo amesababisha timu hiyo kufanya vibaya na kua na wakati mgumu kwenye kupata matokeo.

Klabu ya Atletico Madrid ambayo inatarajiwa kucheza na klabu ya Elche siku ya Jumatano kocha Simeone anasema “Tuna kikosi kizuri, wachezaji wanne kwenye fainali ya kombe la dunia nafikiri kama mwalimu ndo nahitajika kuongeza ubora ili tuweze kurudisha ushindani kwenye La liga”simeoneKocha Simeone ameongeza kwa kusema kua kikosi ambaco walishinda nacho ubingwa msimu wa 2020/21 wachezaji wote wapo kasoro Kieran Trippier na Luis Suarez, Hivo inaonesha bado wana kikosi cha ushindani kugombania taji la La liga.

Acha ujumbe