Todibo Kuondoka Nice Mwishoni mwa Msimu

Beki wa klabu ya OGC Nice na timu ya taifa ya Ufaransa Jean Clair Todibo atatimka ndani ya timu hiyo mwishoni mwa msimu huu na vilabu kadhaa vikitajwa kuwania saini yake.

Klabu ya Nice inaelezwa imeweka wazi dau la beki huyo wazi kwamba atapatikana kwa dau la paundi milioni 40, Hivo kwa klabu ambayo itakua inahitaji huduma ya beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa inatakiwa kufikia dau hilo.TodiboManchester United ni moja ya timu zinatajwa kuwania saini ya Jean Clair Todibo tangu dirisha lilomalizika lakini hawakufanikiwa kuinasa saini ya beki huyo, Hivo dirisha kubwa lijalo inaweza kua nafasi ya klabu hiyo kupata saini ya beki huyo.

Klabu ya Manchester United haitakua vitani yenyewe kwenye vita ya kuwania saini ya beki huyo, Kwani kuna vilabu kadhaa vinavyoshiriki ligi kuu ya Uingereza vinamfatilia beki huyo ili viweze kupata saini yake katika dirisha kubwa lijalo.TodiboBeki Jean Clair Todibo amekua na kiwango kizuri sana ndani ya klabu ya OGC Nice jambo ambalo limefanya vilabu kadhaa kuhitaji saini yake huku Man United wakiwa  wanatajwa zaidi kama moja ya vilabu vinavyohitaji saini yake mwishoni mwa msimu huu.

Acha ujumbe