Kiungo wa timu ya Taifa ya Italia na PSG Marco Verratti atasaini mkataba mpya na timu ya Ufaransa kama ambavyo ilitarajiwa huku akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne ijayo.

 

Verratti Kuendelea Kuitumikia PSG

Mkataba wake mpya unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na wababe hao wa Ligue 1 bado wanahitaji huduma ya kiungo huyo kuendelea kusalia kutokana na kiwango chake kziuri ambacho anazidi kukionyesha.

Verratti na Taifa lake la Italia walishindwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar licha ya kuchukua taji la Uropa baada ya kumuondoa Uingereza kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kuisha kwa sare.

Verratti Kuendelea Kuitumikia PSG

PSG wapo nafasi ya kwanza huko Ligue 1 baada ya kucheza michezo 15, ushindi mara 13, wakiwa wamepata sare mbili pekee na hawajapoteza mchezo wowote hadi sasa.

Baada ya michuano ya Kombe la Dunia kuisha Verratti na wenzake watacheza mchezo wao wa raundi ya 16 dhidi ya Strasbourg ambao wapo nafasi ya 19.

Verratti Kuendelea Kuitumikia PSG

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa