Ni Willy Sagnol, winga ya kulia na ndoto za Wafaransa hapa, kumbuka tupo ndani ya dakika 30 za nyongeza za fainali ya kombe la dunia Ujerumani mwaka 2006. Waitaliano wamefanya kosa la kaburi hapa, wamemuacha Zinedine Zidane kwenye box mwenyewe. Huyu full back wa Bayern Munich ni hatari kwa kumwaga maji, lazima ameshamuona Zidane.
Anaweka krosi moja safi juu ya kichwa cha Zidane, hakika hili ni bao la ushindi kwa Ufaransa. ila hapana, mkono wa kulia wa Gianluigi Buffon upo imara kuwaweka Italia salama hapa. Sasa badala ya bao wafaransa watapiga kona. Buffon anasema hiyo ndiyo save bora aliyowahi kuifanya kwenye maisha yake. Mikono yake ilifanya Waitaliano waondoke na kombe lao la 4 la dunia.

Huyo ndiyo Gianluigi Giggi Buffon. Alianza kulinda milingoti pale Parma miaka 24 iliyopita. anadaka mpaka leo na miaka yake 42. Aliiongoza Parma na njaa zao mwaka 1999 kutwaa Coppa Itallia, Uefa Cup na supercopa Itallia. Aliwatoroka mwaka 2001 na kusaini kwa wakongwe wa Turin.
Mwanaume na gloves zake, mwanaume mbele ya nyavu zake, nyuma ya Fabio Cannavaro, Gianluca Zambrota na Federico Balzaretti waliweka rekodi ya kwenda hadi dakika 970 pasipo kuruhusu bao ndani ya Serie A. Mechi 12 mfululizo pasipo kufungwa, wanaume wale . Muulize Thiery Henry alichokiona mbele yao. Muulize Shevchenko alichokutana nacho na Ac Millan yake
Gianluigi Buffon alikuja kuiaminisha dunia kuwa hata magolkipa wanaweza kuwa bora mbele ya wachezaji wa kati. Golkipa wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Serie A. Golkipa wa kwanza kuondoka na tuzo ya mchezaji bora Ulaya.
Waitaliano wao wanamuita superman. Golkipa bora wa msimu wa serie A mara 12. Binadamu aliyevaa jezi ya timu ya Italia mara nyingi zaidi. Mara 176. Ameenda nao makombe 5 ya dunia. Ametwanga Juve miaka 17 mfululizo.
Wataalam wa soka wanakuambia huwezi kutaja makipa 5 pasipo jina lake, labda uwe na element za uchawi. Pele alimjumuisha kwenye list ya wachezaji 100 bora wanaoishi. Zunguka Italy nzima, waulize watoto wote kwenye academy za soka role model wao. Watakuambia superman Buffon, hata ambao hawana ndoto za ugolkipa.



Issa
Buffon kipa mahiri sana sema kakosa champion league