Hazard: Nilisikitika Mourinho Kutimuliwa

Eden Hazard amefichua kuwa alimtumia ujumbe Jose Mourinho akimuelezea masikitiko yake baada ya meneja huyo kutimuliwa kazi pale Chelsea mwaka 2015.

Mourinho alitimuliwa kazi baada ya kuchapwa na Leicester City bao 2-1 kuelekea mwezi disemba mwaka 2015. The Blues walianza vibaya ligi kwa kushinda gemu 3 tu kati ya gemu 12 za ligi wakiwa pointi moja tu kutoka kwenye ligi.

Hazard: Nilisikitika Mourinho Kutimuliwa
Hazard anaamini alicheza chini ya kiwango Mourinho alivyotimuliwa

Mourinho aliamini wachezaji wake walimsaliti kwenye dimba la King Power, Hazard, Fabregas na Diego Costa walikosolewa sana wakati huo.

Hazard anasema nini?

β€œNilimtumia ujumbe kuwa nasikitika ameondoka, tungefurahia mafaniukio yale yote pamoja lakini hadi sasa haikuwezekana. Nilijiona mkosaji, kwa sababu ningekuwa mchezaji wa mwaka. Nilikuwa mmoja wa wachezaji waliozuga, nilicheza chini ya kiwango.”

Acha ujumbe