Baada ya Monaco kutemwa kwenye michuano ya Coupe de France na klabu ya Metz ambayo inashiriki League 2, Thierry Henry anasema anaihofia zaidi hatma ya klabu hiyo kuliko hatma yake binafsi kama meneja klabuni hapo.
Henry alichukua kibarua klabuni hapo mwezi oktoba mwaka jana, lakini imekuwa vigumu kwake kurejesha mapema tabasamu la mashabiki na tumaini la klabu hiyo. Klabu hii inafurukuta kujiondoa kwenye mstari mwekundu wa League 1 wakiwa nafasi ya 19, wamepata pointi 15 tu kwa gemu 21 walizocheza.
Wakipoteza gemu dhidi ya Metz, magoli ya Hein na Marvin Gapka yaliwasaidia Metz kuondoka na ushindi wa bao 3-1 kwenye dimba la Stade II jumanne na kuwatoa Monaco kwenye michuano ya Ligi hiyo. Goli la kufutia machozi la Monaco lilipatikana baada ya Radamel Falcao kutumia vyema krosi kutoka kwa Djibril Sidibe.
Nyota huyu wa zamani, ambaye pia aliwahi kuichezea klabu hiyo alipoulizwa kuhusu hatma yake klabunihapo akajibu kuwa yeye hana haja ya kufikmiria kuhusu hatma yake, isipokuwa anahofia kuhusu hatma ya klabu hiyo, kuhusu yeye anaamii wamiliki wa klabu hiyo wataamua kuhusu hatma yakle wakati wa kuamua ukifiaka.

