Kwanza tuanze na visiwa flani vilivyotengwa, visiwa hivi kule Carribean Marekani ndipo nyumbani kwa Baba yake Mzazi Thierry Henry aliyekimbia ugumu wa maisha na kuangukia Les Ulis, viunga vya jiji la Paris nchini Ufaransa. Hakuna aliyewahi kujua kama Mtoto kutoka visiwa vile atakuja kutikisa soka la dunia, Mwamba ndiye aliye tinga namba 14 mgongoni, kazi yake  kubwa ilianzia pale visiwa vya Monaco akiwa na umri wa miaka 17 tu, aliyecheza na kuburudisha watu kupitia mpira.
, THIERRY HENRY: Mchawi Mweusi Kutoka La Desirade  ‘Visiwa vya Karibean”, Meridianbet
Ujio wa Henry pale Arsenal

Henry hakupata sifa kubwa sana zaidi ya ujio wake pale Arsenal, 1999 mtoto mmoja akiwa na tabasamu pana kila muda akimwaga wino Highbury mbele ya Makamu Mwenyekiti David Dein, jioni ile mashabiki wa Arsenal walimuwaza zaidi Davo Suker kutoka Madrid kuliko Thiery . Ndani ya Highbury Henry alifanikiwa kushika hisia za mashabiki wengi wa soka, hakuwa tu mfungaji bali mkimbiaji bora zaidi wa mpira “balletic and athletic footballer” akizifanyia kazi pass murua za Mholanzi Dennis Bergamp,

Licha ya mabao 228 pale Arsenal na ubora wote lakini Ufaransa hapewi heshma yoyote, licha ya kujengewa sanamu pale Emirates ila Paris waligoma kumpa heshma, wao wanakutajia Raymond Kopa, Michel Platini na Zinadine Zidane kama wachezaji wao bora wa muda wote

, THIERRY HENRY: Mchawi Mweusi Kutoka La Desirade  ‘Visiwa vya Karibean”, Meridianbet

Wafaransa wanasema “Je t’aime, non plus” kwa Kiswahili ni kuwa Nakupenda ila hunipendi, Henry alifanya makubwa kwenye soka ila Wafaransa wanasema hana hadhi kubwa kwa soka lao, sanamu pekee Ufaransa ni la Zizzou akimpiga kichwa Materrazi lilibuniwa na Abdel Abdessemed

Henry hana furaha kubwa Paris, hana furaha kubwa na viunga alivyoazaliwa, dunia nzima furaha ya Thiery ipo North London, pale Emirates ndio maskani yake, sehemu aliyopata umaarufu wake, alikua kipande kikubwa kwenye jengo la Invicibles ya 2003/04, ni straika bora zaidi kuwahi kutokea pale EPL.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa