Meneja wa Man United, Jose Mourinho ndio anayegonga vichwa vya habari za soka kwa sasa. Mourinho ambaye anadaiwa kuwa kikaangoni tokea alipopoteza gemu dhidi ya Briton, na kukosa bahati zaidi kwa kichapo kilichofuatia akiwa kwake dhidi ya Spurs.
Matokeo mabaya kutoka kwa Briton na Spurs yamekuwa mwiba kwa Mourinho kuliko wakati wowote tangia alipoanza kazi katika klabu hiyo. Mourinho amesisitiza kuwa anahitaji heshima kutokana na ukweli kuwa ameshinda mataji mengi.
Kunaweza kuwa na hali gani Old Traford?
Kiuhalisia, kwa mtazamo wa nje hali inaonekana kuwa mbaya kwa upande wa Mourinho, lakini vyanzo vya ndani ya klabu hiyo vimesisitiza hali ni shwari tuu kila mtu anafanya kazi kwa nafasi yake na jitihada za kufanya vyema zinaendelea.
Lakini kuna hofu ambayo inaendelea ndani ya klabu hiyo na hakuna mtu anayetaka kuwajibika kutokana na nafasi ambayo klabu imejikuta ipo. Baadhi ya wachezaji wanadai wanachanganywa na mbinu za Mourinho na uchaguzi wake wa kiholela wa timu, wapo wanaohisi hawatakua tayari kucheza chini ya mourinho katika msimu ujao.
Duru zinadai kama kuna kushindana kwa ajili ya madaraka basi ni wazi mourinho atashindwa yeye katika klabu hiyo, msisitizo unawekwa kwa bosi huyo kutafuta mbinu mbadala ya kupata ushindi na kuikwamua timu katika nafasi ambayo wanajikuta wapo kwa sasa.
Bodi ya klabu hiyo bado ina imani na Mourinho, wanaamini bado anaweza kubadilisha hali katika klabu hiyo. Mourinho anahitaji umakini zaidi katika kuchagua na kupanga kikosi chake. Mwisho wa Mourinho unaweza kuwa 2020 baada ya mkataba wake kuisha kama hataongeza mkataba lakini kwa sasa bado hali haiko wazi kwa hatma ya mourinho ukiacha mitazamon ya watu.
Povel tz
Habar njema