INONGA RASMI KUKIPIGA MOROCCO MSIMU UJAO

BEKI wa zamani wa Simba ya Tanzania, Henock Inonga anatajwa kuwa kwenye changamoto mpya ndani ya AS FAR Rabat kwa ajili ya kutimiza majukumu yake hapo.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Inonga ndani ya ligi alicheza mechi 10 pekee za ligi muda mwingi alikuwa akitumia kwenye matibabu kwa kuwa hakuwa fiti.inongaInonga anatua AS FAR Rabat timu ambayo ilikuwa ikinolewa na aliyekuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi anayetajwa kuwa alipendekeza jina la mwamba huyo kuwa katika timu hiyo.

Inonga alipewa Thank You na Simba na aliwaaga mashabiki na kushukuru uongozi kwa kumpa nafasi ya kuwa katika kikosi hicho ambacho kwa sasa kimeweka kambi nchini Misri kwa maandalizi ya msimu wa 2024/25.

Nabi kwa sasa ametimkia kunako Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo inatarajia kukutana na Yanga kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kuchezwa Julai 28, Afrika Kusini.

Acha ujumbe