Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema jana ameifikisha tuzo yake katika uwanja wa Santiago Bernabeu mbele ya mashabiki wa klabu hiyo zaidi ya elfu sabini na tano.
Mshambuliaji huyo jana alifanikiwa kuifikisha tuzo yake ya mchezaji bora wa dunia inayojulikanan kama Ballon Dor katika dimba hilo la nyumbani la klabu hiyo ili kuwashukuru mashabiki wa klabu hiyo waliompa ushirikiano kwa kipindi chote alichokua klabu hapo.
Kivutio kikubwa katika tukio hilo ni waliomkabidhi tuzo ambao ni magwiji wa klabu hiyo waliowahi kubeba tuzo hiyo Benzema pia nao ni Zinedine Zidane pamoja na Luca Modric kitu kilichowavutia zaidi mashabiki wa klabu hiyo na wadau wa soka pia huku tuzo ya golikipa bora aliyochukua golikipa bora akikabidhiwa na Iker Casilas golikipa bora pia wa zamani alieitumikia klabu hiyo.Katika hilo lilifanyika jana Bernabeu pia kuna mchezo ulipigwa hapo kati ya wenyeji dhidi ya Sevilla ambapo Madrid walishinda goli tatu kwa moja na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Hispania.
Katika mchezo Benzema hakuweza kushiriki kutokana na maumivu ya misuli aliyoipata siku ya ijumaa mazoezini wakijiandaa kucheza mchezo huo dhidi ya Sevilla.