Mchezaji wa Man United, Jesse Lingard ambaye aliponesha kiwango safi baada ya kujiunga na West Ham United, ameonesha ukomavu katika soka. Ama hakika, uungwana ni vitendo.

Lingard alimaliza msimu wa EPL 2020/21 kwa kupachika magoli 9 katika michezo 16 aliyowatumikia The Hammers. Licha ya kuonesha ubora wake, Jesse Lingard amejikuta akiachwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kitachoshiriki mashindano ya Euro 2020.

Kocha Gareth Southgate alimjumuisha Lingard kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 33 kabla ya kumuondoka kwenye kikosi cha wachezaji 26 watakaopeperusha bendera ya nchi hiyo kwenye mashindano hayo kuanzia Ijumaa hii.

Jesse Lingard

Licha ya kutochaguliwa kwenye kikosi cha Euro 2020, Jesse Lingard alipatiwa nafasi ya kucheza michezo 2 ya kirafiki na sasa ni rasmi, Lingard ataishuhudia michezo hiyo akiwa nyumbani.

Yote 9, Jesse Lingard ameamua kuweka wazi hisia zake kupitia mtandao wa Twitter ambapo ameweka chapisho lililosomeka ” Linapokuja suala la kuwasapoti wachezaji wenzangu na kuiwakilisha nchi yangu, sitoacha kutabasamu.

“Nitaisapoti timu yangu muda wote! Kila la kheri kwa wachezaji wote! Leteni kombe nyumbani!”

Swali la kujiuliza ni je, United wataendelea kumbakiza Lingard Old Trafford au watamuuza kwenye dirisha hili la usajili?


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa