KIKOSI cha KMC kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Arta Solar 7 ya nchini Djibouti, Agosti 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Kikosi hicho cha KMC ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thierry katika mechi mbili za ligi kuu kimefanikiwa kukusanya pointi moja katika mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania.

kmc, KMC Kujipima Nguvu na Arta Solar 7, Meridianbet

Akizungumzia mchezo huo, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa “Kwa sasa wachezaji wamepewa mapumziko na siku ya kesho jumatano watarejea kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo.

“Hao wa Djibouti ndio wametuomba mchezo wa kirafiki kwa sababu wapo hapa mjini lakini hata kwa upande wetu sisi tulikuwa tunahitaji mchezo wa kirafiki ili tujipime.

“Katika kipindi hiki cha mapumziko mafupi kocha atapata muda wa kukitengeneza vizuri kikosi chake na kuona ni namna gani yale mapungufu aliyoyaona kwenye michezo miwili tuliyocheza yanarekebishwa.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa