Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Julian Nagelsmann amethibitisha kuwa mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz atajumuishwa kwenye kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Havertz amemaliza msimu kwa mafanikio makubwa licha ya kukumbwa na majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amesaidia Arsenal kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na kumaliza ukame wa miaka 22 bila taji hilo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mjerumani huyo amecheza michezo 11 pekee ya Ligi Kuu England msimu huu, lakini ameonyesha kiwango bora katika mechi za hivi karibuni. Havertz alifunga bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Burnley na pia alitikisa nyavu kwenye mchezo dhidi ya Manchester City uliomalizika kwa Arsenal kupoteza mabao 2-1.
Baada ya kusherehekea ubingwa wa England, Havertz sasa ataelekeza nguvu zake kwenye Kombe la Dunia baada ya Arsenal kumaliza mechi zao zilizobaki dhidi ya Crystal Palace pamoja na fainali ya UEFA Champions League Final dhidi ya Paris Saint-Germain.
Nagelsmann amesema ana imani kubwa na mshambuliaji huyo ambaye anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Ujerumani kama namba tisa katika michuano hiyo mikubwa duniani.
“Ukiwa uwanjani wewe ni mchezaji wa kipekee na muhimu sana kwetu. Endelea kuwa na afya njema, tuliza akili yako na pambana. Una kila kitu tunachohitaji ili kuwa na mshambuliaji bora wa mbele,” alisema Nagelsmann.


