Marcelo Atajwa Kuwa Mmoja ya Makocha Wajao wa Uruguay

Marcelo Bielsa anaripotiwa kuwa katika kinyang’anyiro cha kuchukua nafasi ya Diego Alonso kama kocha ajaye wa Uruguay baada ya timu hiyo ya Amerika Kusini kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia katika hatua ya makundi. Machaguo spesho ya kombe la dunia yapo kwaajili yako Meridianbet.

 

marcelo

Uruguay walifanikiwa kuifunga Ghana katika mchezo wao wa mwisho wa kundi siku ya Ijumaa, lakini bao lililofungwa na Korea Kusini katika mechi nyingine ya Kundi H lilimaanisha kwamba timu ya Alonso ilitoka kwenye michuano hiyo kwa mabao ya kufunga. Beti na kitochi mechi ya hatua ya 16 bora Meridianbet.

Wakiwa na matumaini makubwa kuelekea Qatar, Kombe la Dunia la Uruguay limemalizika mapema zaidi, huku timu hiyo ikifunga mabao mawili pekee katika mechi zao tatu, na kumwacha Alonso katika hatari ya kupoteza kibarua chake.

 

marcelo

Iwapo Uruguay itaamua kufanya mabadiliko dimbani, Bielsa anaaminika kuwa chaguo ambalo wanazingatia, kwa mujibu wa TyC Sports.

Marcelo anafahamika zaidi nchini Uingereza kwa miaka minne aliyoichezea Leeds, ambayo ilimfanya arudishe klabu hiyo kwenye Ligi kuu baada ya miaka 16 kutoshiriki ligi kuu.

Muargentina huyo alipendwa sana na mashabiki wa klabu hiyo, lakini aliachishwa kazi mwezi Februari baada ya matokeo mabaya.

 

Marcelo

Hivi majuzi alihusishwa na kurejea Ligi Kuu ya Uingereza kuinoa Bournemouth, lakini mazungumzo yalikwama, na timu hiyo ya Pwani Kusini sasa imemweka Gary O’Neil kuwa kocha wa kudumu baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika kipindi chake cha muda akiwa usukani.

Iwapo Marcelo Bielsa atapata kibarua cha Uruguay, hautakuwa mradi wake wa kwanza katika usimamizi wa kimataifa.

Aliifundisha Argentina kwa miaka sita kati ya 1998 na 2004, akishinda medali ya dhahabu ya Olimpiki.

Pia aliiongoza Chile kuanzia 2007 hadi 2011, na kuifikisha timu hiyo katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la 2010 kabla ya kuondolewa na Brazil.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Acha ujumbe