Picha zilizovuja zimeonyesha kocha wa Cameroon Rigobert Song akifichua jinsi mlinda mlango wake aliyefukuzwa Andre Onana alilia na kukataa kuzungumza naye kabla ya kurejeshwa nyumbani kutoka kambi yao ya Kombe la Dunia.

 

onana

Song na Onana walihusika katika ‘mzozo mkali‘ wakati walipokuwa Qatar huku ikiripotiwa kuwa walizozana kuhusu staili za walinda mlango, huku kocha huyo akikosa kufurahishwa na mchezaji wake nambari 1 kucheza mchezo wa kuhatarisha lango lake.

Ni maneno ya ukali ndiyo yaliyoanza, huku Onana akisisitiza kuwa hatabadili mtindo wake. Baadaye aliondolewa kwenye kikosi chao na nafasi yake kuchukuliwa na Devis Epassy, ambaye aliruhusu mara tatu katika sare ya 3-3 dhidi ya Serbia.

Sasa Song ameelezea kwa undani kile kilichosemwa wakati wa majadiliano yao ya wakati huo baada ya kuvuja kwa kipande cha picha yake akielezea hali hiyo kwa kile kinachoonekana kuwa ni moja ya makocha wenzake wa timu hiyo.


“Siku ya mchezo na Serbia nilimwambia Onana kuwa nilihitaji kuzungumza naye na akaanza kulia,” Song alisema kwenye video hiyo.

“Nilimwambia, “Sina muda wa kujadili masuala haya. Nilikupigia simu jana na hukuzungumza nami. Nilifanya mazungumzo na Aboubakar, Choupo-Moting na Anguissa, ambao ni wachezaji wawakilishi zaidi katika timu; kwa nini nisiongee nawe?”

“Onana anafanya vizuri katika mazoezi lakini anahatarisha sana wakati wa michezo. Nilimwambia mara kwa mara, “Hupaswi kuchukua hatari. Pitisha mpira pembeni, sio katikati”.

 

onana

“Aliniambia, “Ninacheza, sina muda wa kuzungumza nawe”. Alipokuwa hotelini, hakuzungumza nami, lakini alikwenda kwa Rais Samuel [Eto’o] na akampeleka sijui wapi.”

Song baadaye alisema uamuzi wake wa kumrudisha nyumbani ulikuwa ‘kwa manufaa ya timu, ikizingatiwa kwamba heshima yake [nchini] Cameroon ilikuwa imevunjwa’.

Kuondolewa kwa Onana kwenye timu ya Cameroon ni utata wa hivi punde zaidi unaohusisha kipa huyo, ambaye mwaka jana alitumikia marufuku ya miezi tisa kwa kukiuka kanuni za matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Awali Onana alipigwa marufuku kwa muda wa miezi 12 baada ya kufeli kipimo cha dawa lakini adhabu hiyo ilipunguzwa na miezi mitatu baada ya UEFA kukubali kuwa alikosea kutumia kidoge kimoja cha mkewe kwa maumivu ya kichwa.

Onana pia alipata ajali ya gari mwezi Machi mwaka huu alipokuwa akielekea kuungana na timu ya Cameroon akiondoka bila majeraha, kabla ya kuanza kuichezea timu yake katika mechi ya mtoano ya Kombe la Dunia dhidi ya Algeria.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa