Klabu ya Ac Milan kuwakaribisha klabu ya As Roma leo katika mchezo wa ligi kuu soka nchini Italia maarufu kama Serie A mchezo utakaopigwa katika dimba la San Siro.

Klabu ya Ac Milan leo watakua wana nafasi ya kuendelea kupunguza pengo la alama baina yo na klabu ya Napoli ambao ni vinara wa kigi hiyo, Kwasasa klabu hiyo ipo nafasi ya tatu wakiwa na alama 36 hivo kama watashinda mchezo watakwenda kushika nafasi ya pili wakiwa na alama 39 huku Napoli wakiwa na alama 41.ac milanMabingwa watetezi wa Italia klabu ya Ac Milan ambao hawakuuanza msimu vizuri lakini kwasasa wanaonekana kua kwenye kiwango kizuri, Klabu hiyo imefanikiwa kushinda mchezo wake wa kwanza wa Serie A tangu kurejea kwa ligi hiyo huku vinara wa ligi wakipoteza dhidi ya klabu ya Inter Milan.

Klabu ya As Roma chini ya Jose Mourinho wao watakua ugenini kuhakikisha wanapata alama dhidi ya mabingwa hao watetezi katika dimba lao la Sa Siro. As Roma wao wanakamata nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi hiyo hivo ni wazi watakua wahitaji kupata alama tatu ili kusogea kwenye nafasi nne za juu.ac milanMchezo huo unatarajiwa kua mkali na wenye mvuto kwani zinakutana timu zenye ubora mkubwa na zenye historia kubwa kwenye soka la Italia, Vilevile inakutanisha makocha wenye uwezo nkubwa Stefano Pioli kwa upande wa Ac Milan na Jose Mourinho upande wa As Roma.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa