Miamba ya soka kutoka nchini Italia vilabu vya Ac Milan pamoja na Juventus leo vitashuka dimbani kumenyana katika mchezo wa ligi kuu ya Italia Seria A.
Timu zote ziko kwenye nafasi za nne za juu katika msimamo wa ligi kuu Italia na mchezo wa leo utakaokwenda kupigwa katika dimba la San Siro ambapo Ac Milan watakua nyumbani kuhakikisha wanatafuta uongozi wa ligi hiyo.Vilabu hivo vinafatana katika msimamo wa ligi kuu ya Italia ambapo Ac Milan wanakamata nafasi ya pili, Huku Juventus wakiwa nafasi ya tatu na wakipishana kwa alama nne hivo Juventus watahitaji kupata matokeo ili kupunguza pengo la alama baina yao.
Timu zote mbili zimekua na matokeo mazuri siku za karibuni na ndio sababu ya kuakamata nafasi za juu mpaka sasa, Hivo katika mchezo wa leo kila mmoja atahitaji kuhakikisha anaendeleza matokeo mazuri.Klabu ya Juventus wanahitaji kushinda mchezo wa leo ili angalau kupunguza pengo la alama mpaka kufikia alama moja, Wakati huo Rossoneri watahitaji alama tatu ili kukaa juu ya kilele cha msimamo wa Serie ambapo mpaka sasa vinara ni klabu ya Inter Milan.