AC Milan Kusepa na Watatu 3 Chelsea.

Klabu ya AC Milan inaendelea ilipoishia msimu uliopita linapokuja suala la usajili barani Ulaya.

Milan wamemaliza msimu wa Serie A wakiwa nyuma ya majirani zao Inter katika msimamo wa Ligi hiyo na sasa wanajiandaa kukisuka kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Inaripotiwa kuwa, AC Milan imefikia makubaliano ya kumsajili Olivier Giroud kwa mkataba wa miaka miwili. Licha ya Giroud kusaini mkataba wa mwaka 1 kuendelea kuwepo Stamford Bridge, bado hatma yake klabuni hapo kwa msimu ujao haijulikani.

Sambamba na Giroud, Milan wanamuwinda Hakim Ziyech ambaye wanamuona kama mbadala sahihi wa Hakan Calhanoglu ambaye ametimkia Inter kama mchezaji huru. Milan pia wanampango wa kurudi kumchukua Tiemoue Bakayoko ambaye aliitumikia klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita.

Fikayp Tomori

Endapo AC Milan watafanikiwa katika hili, watakuwa wamechukua jumla ya wachezaji 4 wa Chelsea kwa misimu miwili ikiwa ni pamoja na Fikayo Tomori ambaye wamekamilisha usajili wake wa moja kwa moja.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe