Klabu ya Ac Milan inayoshiriki ligi kuu nchini Italia ipo kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba kiungo wake raia wa Algeria Ismael Bennacer.

Kiungo Ismael Bennacer amekua kwenye kiwango bora sana tangu ajiunge na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Italia Serie A, Klabu hiyo imefikia uamuzi wa kutaka kumuongezea mkataba mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria.ac milanKiungo huyo ambaye amebadilisha wakala siku za hivi karibuni klabu ya Ac Milan imepanga kufanya mazungumzo na wakala wake mpya Enzo Raiola ili kujadili mkataba mpya wa mchezaji huyo ambao unamalizika mwaka 2024.

Kikosi cha Ac Milan chini ya kocha Stefano Pioli kimekua kikifanya vizuri na baada ya kubeba ubingwa wa ligi hiyo msimu uliomalizika, Imekua utaratibu wa klabu hiyo kutaka kuwaongezea mikataba wachezaji wake muhimu ili kuifanya klabu hiyo kuendelea kufanya vizuri kwa siku zijazo.ac milanKiungo Ismael Bennacer ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye mradi wa muda mrefu wa klabu ya Ac Milan ambao inataka kuufanya, Hivo klabu hiyo inapanga kumuongezea mkataba mpya ili aweze kusalia klabuni hapo kwa muda mrefu ili mradi wa klabu hiyo uweze kukamilika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa