Wakati zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya klabu ya As Roma kutangaza kuwa Jose Mourinho atakuwa kocha wao kuanzia msimu ujao, kocha huyo ameanza mipango ya kunoa kikosi chake kuelekea kwenye kuhakikisha anakuwa na kikosi bora sana msimu ujao kwa kutoa pendekezo la kwanza.
Mourinho amemtaja mchezaji beki kisiki wa Brighton kama chaguo lake la kwanza la usajili wa kuongeza katika kutengeneza timu itakayopigania taji la Serie A msimu ujao pale Italia.
Ben White amekuwa miongoni mwa walinzi bora sana msimu huu akiwa na Brighton. Amefanikiwa kucheza mechi 33, ndani ya dakika 2925 na kuweka angalau clean sheets 12 kati ya mechi 32.

Endapo Roma watafanikiwa kuchukua saini ya Ben White, basi maisha ya mabeki wake wa kati Gianluca Mancini na Marash Kumbulla yatakuwa magumu sana kwa kuzingatia ukweli kuwa Mourinho huwa anatabia za kuwapendelea wachezaji fulani kila anapoingia klabu fulani.
Mourinho alifukuzwa pale Tottenham hivi karibuni kutokana na kile kilichodaiwa kuwa alipinga sakata la European Super League na kuwaacha Tottenham wakiwa hawaelewi ni kocha gani sahihi wa kumsajili mpaka sasa.
Mourinho amekuwa sio mtu wa kukaa sana kwenye timu kwa muda mrefu kila anapoingia na ametajwa kuwa kocha aliyekusanya pesa nyingi sana kwa kufukuzwa tu ama kuvunjiwa mikataba na timu anazoajiriwa.
Je, Nguli huyo atakaa Roma kwa muda gani na atafanikisha kunyaka saini ya Ben White ambaye ameanza kutolewa macho na klabu mbalimbali za Uingereza hivi sasa?
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Inaonekana kocha atafanya mambo mazuli sana
Habari njema hiyo jose kila raheri katika mapambano
Ngoja tuone Mourinho kama ataweza kuinoa ac roma
Kocha yuko vizur
Mambo 🔥🔥🔥
Habar njema
Safii
Kocha yuko vizuri
Mourinho anajua kuchagua
Mambo ni moto
Kocha yupo vzr
Kocha yupo vizuri