Kiungo wa kati wa Milan Ismael Bennacer amesaini mkataba mpya wa muda mrefu na mabingwa hao watetezi wa Serie A ambao utaendelea hadi Juni 2027.
Bennacer mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Milan kutoka Empoli Julai 2019 na ameichezea klabu hiyo mechi 129.
Ameshiriki katika mechi zote 24 za Rossoneri msimu huu akiwa ni mmoja wa wachezaji wawili pekee waliowahi kuibuka na ushindi pamoja na Pierre Kalulu.
Mkataba wa Bennacer ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu ujao, lakini mkurugenzi wa ufundi wa Milan Paolo Maldini alithibitisha wiki hii kuwa mkataba mpya ulikuwa karibu kukamilika.
Milan walitangaza kwenye tovuti yao rasmi siku ya jana kwamba mchezaji huyo wa Kimataifa wa Algeria sasa yuko chini ya mkataba wa miaka mingine minne na nusu.
Kikosi cha Stefano Pioli, ambacho kiko pointi saba nyuma ya vinara Napoli, pia kina matumaini ya kumfunga Rafael Leao huku kukiwa na taarifa za kutakiwa kutoka kwa vilabu vingi vikubwa.