Kiungo wa klabu ya Ac Milan Ismael Bennacer raia wa kimataifa wa Algeria amesaini kandarasi mpya ya kuendelea kuitumikia klabu ya Ac Milan Mpaka mwaka 2027.

Kiungo Bennacer alikua anafanya mazungumzo n klabu ya Ac Milan kwa wiki kadhaa nyuma ili koungeza mkataba na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Italia Serie A. Mazungumzo baina ya mchezaji huyo na klabu ya Ac Milan yamemalizika na mchezaji huyo ataendelea kusalia klabuni hapo kwa muda mrefu.bennacerIsmael Bennacer amekua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Ac Milan chini ya kocha Stefano Pioli, Hivo klabu hiyo ikaona umuhimu wa kiungo huyo na kuamua kumuongezea mkataba aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo.

Kocha wa klabu ya Ac Milan ni mtu ambae amehakikisha kua mchezaji huyo anasalia ndani ya viunga vya Milan, Kwani kocha Pioli ndio alipendekeza kiungo huyo aongezewe mkataba kwani ni miongoni mwa wachezaji ambao ni muhimu kwenye mipango yake.bennacerKiungo Ismael Bennacer amesaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Ac Milan ambao utamueka klabuni hapo mpaka mwaka 2027, Lakini kwenye kipengele cha mkataba wake mchezaji huyo ataruhusiwa kuuzwa kama klabu yeyote itafika kiasi cha Euro milioni 50 ambayo ndio itakua thamani ya kuvunja mkataba wa kiungo huyo ndani ya Milan.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa