Taarifa kutoka nchini Italia zinadai kuwa nyota wa Juventus, Gleison Bremer atafanyiwa upasuaji wa goti mjini Lyon leo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alipata jeraha mbaya katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya RB Leipzig wiki iliyopita.
Tuttosport na Gazzetta dello Sport, siku ya leo, zinaripoti kwamba beki huyo wa Brazil alikwenda Lyon kwa ziara ya kitaalam na amebaki katika jiji la Ufaransa ambako atafanyiwa upasuaji leo.
Juventus walisema wiki iliyopita kwamba Bremer alipata jeraha la anterior cruciate ligament katika goti la kushoto.



