Bremer Akamilisha Upasuaji Wake

Beki wa klabu ya Juventus raia wa kimataifa wa Brazil Gleison Bremer leo amekamilisha upasuaji wake wa goti ambao ameufanya baada ya kupata majeraha wiki iliyomalizika ambayo yatamueka nje ya uwanja mpaka msimu ujao.

Beki Bremer alipata majeraha ya goti (ACL) ambayo yamekua yakiwaandama kwelikweli wachezaji kwasasa ambapo yamemfanya kufanyiwa upasuaji ambao utamueka nje ya uwanja mpaka mwanzoni mwa msimu wa 2025/26 klabu yake ya Juventus imethibitisha jambo hilo.bremerBeki huyo amekua moja ya mabeki muhimu ndani ya klabu ya Juventus lakini kwa bahati mbaya amepata majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja mpaka msimu ujao, Lakini upasuaji ambao ameufanya leo umekwenda vizuri na taratibu za kuanza matibabu ili kurejea kwenye utimamu wake (recovery) yameanza leo rasmi.

Beki Bremer alisaini mkataba mpya mwanzoni mwa msimu huu ambapo ni wazi ataendelea kuwepo ndani ya Juventus kwa muda mrefu zaidi, Lakini beki huyo anaelezwa kufuatiliwa kwa karibu na klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza ambao wanamuona kama mbadala sahihi wa beki wao Virgil Van Dijk.

Acha ujumbe