Mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri anasema Federico Chiesa huenda akaanza dhidi ya Lazio huku mchezaji wa kimataifa wa USMNT Weston McKennie akizidi ‘kutegemewa.’
Allegri alihutubia wanahabari katika mkutano wa kabla ya mechi siku ya jana. Chiesa alikuwa amejiondoa kwenye kikosi cha Italia wiki jana kutokana na jeraha kidogo la misuli lakini inaonekana inafaa kuanza kesho.
Allegri amesema; “Nadhani ana nafasi nyingi za kuanza. Amerudi. Alikuwa amepata nafuu kwa siku chache kisha akarejea mazoezini na timu nyingine ili aanze,” .
Mtaalamu huyo wa Kiitaliano pia alimsifu Manuel Locatelli na McKennie kwa maonyesho yao na Italia na USMNT wakati wa mapumziko ya kimataifa.
Locatelli anaendelea vizuri na amecheza mchezo mzuri. Alihitaji mwito huu na mchezo kama huu. McKennie anaweza kucheza katika safu ya kati au kama winga. Anaweza kuanza kesho.
Allegri amesema kuwa anafanya tathmini juu yake na Danilo ambaye alirejea jana. McKennie anakuwa wa kutegemewa, amefurahishwa na jinsi anavyofanya mazoezini. Ni muhimu kwake kubaki makini kwa msimu mzima.
Kiungo huyo wa kati wa Marekani anaweza kuwa mfungaji wa mkwaju wa penalti dhidi ya Lazio.
Kean ni mpigaji mzuri wa penalti, sawa na Danilo. McKennie, kwa njia yake mwenyewe, anaweza kupiga mikwaju ya penalti pia. Ikiwa atacheza, itakuwa ni mechi yake ya 100, matokeo mazuri kwake.
Akizungumzia wapinzani wa Jumamosi, Allegri alisema: “Lazio wana mbinu nzuri, Luis Alberto, Immobile, Zaccagni, Felipe Anderson, Pedro na Cataldi. Ni wachezaji wa kiufundi na wepesi, wajanja kwenye nafasi zinazobana. Maelezo yatafanya tofauti. Ni mchezo muhimu kesho, Lazio ni mmoja wa wapinzani wetu wa nne bora, ambayo ndio lengo letu kuu.”