Kwenye maisha ya soka, kuna wachezaji wakitoka timu moja kwenda nyingine inakuwa kama ni mkosi. Christian Eriksen wa Inter Millan, sio yule wa Tottenham. Amepatwa na nini?
Maisha ndani ya Inter Millan yamemuendea kombo Christian Eriksen na sasa uwezekano wa kuoneshwa mlango wa kutokea ni mkubwa zaidi. Hii ni baada ya kocha- Antonio Conte na Mkurugenzi wa Inter -Beppe Marotta kutoa tamko kuhusu hilo.
Christian Eriksen alijiunga na Inter Millan mwezi januari akitokea Tottenham ambako alikuwa na wakati mzuri kabla ya maisha kumuwia magumu kidogo baada ya Jose Mourinho kukabidhiwa mikoba ya Mauricio Pochettino.
Kupitia DAZN, Marotta amesikika akisema ” Jana, Conte aliwajibu vizuri zaidi. (hii ni baada ya Conte kuulizwa kuhusu hatma ya Eriksen ndani ya kikosi cha Inter)
“Ninaongezea kwa uwazi kabisa, hatutamzuia mchezaji ambaye ameomba kuondoka. Tutahitaji kufanya tathimini kwa usahihi.
“Conte anamtumia Eriksen kwa heshima ya mchezaji na klabu. Hakuna ofa iliyotufikia mpaka sasa. Tutafanya maamuzi sahihi katika muda sahihi.”
Marotta hajasema kama Eriksen amesababisha matatizo yeyote au kama ameomba kuondoka. Japokuwa, anajaribu kusema kuachana na mchezaji huyo itakuwa ni uamuzi sahihi zaidi.
Eriksen hajaonesha ubora wake ndani ya Serie A na kwa kiasi kikubwa anaonekana kama ni mchezaji wa ziada kwa Antonio Conte. Mchezo dhidi ya Torino wikiendi hii, Eriksen alijikuta akisugua benchi licha ya kufanya vizuri akiwa na timu ya taifa ya Denmark.
Hadi 130,000,000 Tsh kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.
Salma ngende
Duh ilo ni tatizo
Angelina
Nice update
magdalena
unaweza kukuta mchezaji anapoenda timu fulani anakuwa hapati muda wa kupewa nafasi ya kuingia uwanajani
Fatuma kasomo
Asante kwa taarifa meridianbet
Mariam mtandama
Safi
Antony Luseno
Bora arudi zake spurs natumai mourihno atamfaa
Adelta
Bora arud nyumbani tu kumenoga spurs
Sania
Kuhamahama sio poa
Ester jackson
Hii ni changamoto kubwa sana kwa wachezaji mana anajikuta anataka kufanya jambo kubwa ili awe bora lakini hapati nafasi ya kucheza uwanjani hivyo anakata tamaa mwishiwe anaomba kuondoka na kujenga ugovi baina ya kocha na wishoe hupotea zaidi hivyo ni nafikiri wangeweka utaratibu mzuri kila mchezaji angepata kucheza angalau hata kwa dk 15
Sarah
Asante kwa taarifa
Shakila mrope
Asant kwa taarifa meridian bett
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri pengine Yeye pale alivyo toka Ndio kwenda kupata nafasi Nzuri yakukionesha kipaji zaidi
Mwajumah
Safi
Tatu
Safi
Fatina mfingi
Safii
Elika
Safi sana aende tuu
lombo
vzr
Rehema
Gud news
Hopemwaikuka
Safar njema aendako
Povel
Return om Erickson in spurs
aisha
Duuh sio powa
Saupha mohamed
Safari njema
Issa
Inter imemkosa mtu muhimu sana
Sauda
Aende Spurs bado wanamuhitaji.
Janeflora malisa
Safi
samiah
Safi
Rahma
Dar sio poa
warda
Aende tu