De Gea ni Mali ya Fiorentina

Aliyekua golikipa wa klabu ya Manchester United David de Gea amefanikiwa kujiunga na klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi kuu nchini Italia baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

David de Gea ambaye alikaa msimu mzima nje ya soka baada ya kuondoka Manchester United hatimae amefanikiwa kupata timu ambayo ni Fiorentina, Klabu hii imempa mkataba wa mwaka mmoja golikipa huyo ambaye aliondoka ndani ya Man United kama golikipa bora wa msimu wa 2022/23.de geaGolikipa huyo inaelezwa vilabu vingi vilikua vinavizia saini yake lakini maslahi yake ndio yalikua changamoto kwa baadhi ya vilabu, Lakini Fiorentina wameonekana kumpatia kila ambacho alikua anakihitaji golikipa huyo na hatimae atakipiga ndani ya ligi kuu ya Italia Serie A msimu ujao.

Golikipa De Gea amefanikiwa kufika katika jiji la Florence leo kwajili ya kufanya vipimo vya afya na kusaini mkataba rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya Fiorentina, Golikipa huyo amejiunga kwenye ligi kuu ya Italia kama mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu ya Man United Raphael Varane ambaye amejiunga klabu ya Como.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.