Donyell Malen amefichua nafasi kubwa aliyocheza Gian Piero Gasperini katika kumshawishi kujiunga na AS Roma, huku mshambuliaji huyo wa Uholanzi akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kusaini mkataba wa kudumu na Giallorossi hadi mwaka 2030 baada ya kuwa na msimu wa kwanza wa kuvutia sana katika jiji la Rome.

Mchezaji huyo mwenye miaka 27, aliyefunga mabao 14 katika mechi 18 za Serie A na kusaidia Roma kufuzu kucheza UEFA Champions League, alimiminia sifa nyingi kocha aliyefungua uwezo wake baada ya kipindi kigumu akiwa Aston Villa.
“Nini kilinishawishi? Bila shaka jina la Roma na klabu yenyewe, lakini pia malengo ya klabu na kocha wetu,” alisema Malen kupitia Retesport.it. “Tulipozungumza, kwa maneno machache tu alinifanya nijisikie muhimu mara moja na sehemu kuu ya mradi huu.”
Alipoulizwa kama alitarajia kuwa na athari kubwa na ya haraka kiasi hicho katika Serie A, Donyell Malen alionyesha unyenyekevu katika majibu yake.
“Kwa hakika nilitumaini na kutarajia kufanya vizuri. Lakini kama nimefikia kiwango hiki na kufunga mabao mengi namna hii, nawadaiwa zaidi wenzangu wa uwanjani pamoja na kocha ambaye tangu mwanzo aliniweka katikati ya safu ya ushambuliaji.”Alisema



