Uhusiano wa kikemikali kati ya Malen na Dybala umekuwa msingi muhimu wa mfumo wa mbinu za Gian Piero Gasperini msimu huu. Baada ya ushindi dhidi ya Torino katika Uwanja wa Stadio Olimpico Grande Torino.

Malen alifanya haraka kumsifu mchezaji mwenzake huyo wa Argentina kwa mchango wake katika bao la kwanza, akisisitiza uelewano wa asili unaoendelea kujengeka kati yao. Vyombo vya habari vya Italia vimewapa Dybala na Malen jina la “dream duo”, huku wakiunda jina lao jipya la pamoja: “Dybalen”.
“Mshikamano wangu na Dybala? Ni jambo la kufurahisha. Dybala alitoa pasi nzuri sana, na nasikitika kwamba hakupata assist kwa sababu kipa aliugusa mpira. Jambo muhimu lilikuwa kufunga.” Malen aliiambia DAZN
Kwa kufunga bao dhidi ya Torino, Malen amejiandikisha katika historia ya Roma baada ya kusawazisha rekodi iliyowahi kuwekwa na mchezaji bora zaidi kuwahi kuichezea klabu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 sasa amefunga mabao sita katika michezo ya mwanzo ya msimu huu, idadi inayomfanya kusawazisha mwanzo wa gwiji Francesco Totti katika msimu wa 2001-02.
Hii ni rekodi yenye uzito mkubwa katika jiji la Roma, lakini Malen anaonekana kufurahia presha inayokuja kutokana na kulinganishwa na gwiji huyo.

Umuhimu wa takwimu za mwanzo wa msimu wa Malen ni mkubwa sana, kwani amekuwa mchezaji wa tatu pekee katika historia ya Roma kufunga zaidi ya mabao matano katika michezo minne ya mwanzo ya msimu.
Ingawa rekodi ya Totti ya mwaka 2001 ndiyo inayotumika kama kipimo katika zama za kisasa, ni Pedro Manfredini pekee aliyefunga mabao saba katika msimu wa 1960-61, idadi ambayo bado iko juu ya mabao aliyofunga Mholanzi huyo hadi sasa.
“Kuvunja rekodi? Najua jinsi Totti alivyo muhimu kwa Roma. Ninafurahia sana kucheza soka hili na kuvunja rekodi hizi,” aliongeza.
Mbali na mafanikio ya kuvutia ya safu ya ushambuliaji, Gasperini anasimamia kwa umakini kikosi chake ili kuhakikisha kinaendelea kuwa na ushindani katika mashindano yote. Kocha huyo alitetea uamuzi wake wa kumtoa Malen mapema katika kipindi cha pili, akieleza kuwa walihitaji wachezaji wenye nguvu mpya kutokana na ratiba yenye msongamano wa michezo.
“Tunahitaji kila mchezaji katika kikosi hiki kuongeza kiwango chake. Huu ulikuwa mchezo wetu wa tatu ndani ya siku nane, na huwezi kuwa na wachezaji wanaocheza dakika 90 mara kwa mara,” Gasperini alisema.
“Ikiwa tutaweza kuwapa mapumziko ya dakika 20-30, hilo linaweza kuleta tofauti kwa muda mrefu. Pia tunahitaji wale wanaokuja nyuma ya mastaa kama Dybala na Malen kuongeza kiwango chao na kuwa tayari kuchukua nafasi ya kuwa wachezaji muhimu.”
Kwa ushindi wa nne mfululizo, Roma sasa inaelekeza nguvu zake katika kile ambacho wengi wanakiona kama mchezo wa mapema wa kuamua mwelekeo wa mbio za ubingwa dhidi ya mabingwa watetezi, Inter.



