Douglas Luiz Kwenda ni Done Deal

Klabu ya Juventus imemalizana na klabu ya Aston Villa zimemalizana juu ya usajili wa kiungo wa kimataifa wa Brazil Douglas Luiz dili hilo mbali na pesa ila litahusisha mabadilishano ya wachezaji wawili.

Aston Villa watapokea kati €25 mpaka €30 milioni ambapo Juventus watawapa Villa wachezaji wawili katika usajili huu ambao ni Enzo Barrenechea, pamoja na Samuel Illing Jr ambao watakua sehemu ya kukamilisha dili hilo ambalo liko mwishoni kabisa.douglas luizDouglas Luiz ambaye amekua kwenye kiwango bora sana kwa takribani misimu miwili ndani ya klabu ya Aston Villa, Jambo ambalo limekua likizivutia vilabu kadhaa barani ulaya, Lakini klabu ya Juventus ndio wamefanikiwa kukami,isha usajili wa mchezaji huyo.

Kocha mpya wa klabu ya Juventus Thiago Motta inaelezwa ndio ameupa presha uongozi wa klabu ya Juventus kuhakikisha wanakamilisha usajili wa kiungo huyo mapema, Hivo uongozi wa klabu hiyo hawakua na budi kuhakikisha Douglas Luiz anatua kwenye viunga vya Allianz.

Acha ujumbe