Paulo Dybala anahisi Roma inahitajika kutuma ujumbe kwa kuichapa Empoli mabao 7-0 na kukaribisha bao la kwanza la Romelu Lukaku akisema “Hakuna ubinafsi hapa.”

 

Giallorossi walikuwa na pointi moja pekee kutoka kwa raundi tatu za mwanzo na waliingia kwenye mchezo huu bila Lorenzo Pellegrini, Houssem Aouar, Chris Smalling, Tammy Abraham na Marash Kumbulla.


Hata hivyo, waliibomoa Empoli 7-0 na Dybala mabao mawili, bao la kujifunga, pamoja na Renato Sanches, Bryan Cristante, Lukaku na Gianluca Mancini.

“Hakika tulihitaji kutuma ujumbe, kubadilisha kitu na kila mmoja wetu ajaribu kujitolea kwa kutoa kitu zaidi. Nadhani tulifanya hivyo usiku wa leo,” Dybala aliiambia DAZN.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Dybala na Lukaku kuweza kuanza pamoja na wote wawili walilenga goli, ingawa Mbelgiji huyo alizifumania nyavu akiwa amechelewa wakati La Joya akiwa tayari ameshatoka uwanjani.

“Nimefurahishwa na ujio wa Lukaku, Azmoun, N’Dicka na wachezaji wote wapya waliosajiliwa. Nilizungumza na kocha na kujaribu kurejea katika hali nzuri wakati wa mapumziko kwa ajili ya majukumu ya kimataifa, najisikia vizuri leo.”

Dybala alifunga bao la kwanza jana usiku kwa mkwaju wa penalti, lakini kwa kuwa Lukaku pia ana rekodi nzuri katika mazingira haya, je Muargentina huyo atakuwa tayari kushiriki majukumu hayo?

“Hakuna ubinafsi hapa, yeyote anayehisi anataka kupiga penalti ataipiga. Kwa hivyo nitachukua zingine na zingine zitakuwa za wachezaji wenzangu.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa