Fiorentina Yamsajili Moise Kean

Klabu ya Fiorentina kutoka nchini Italia imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Moise Kean raia wa kimataifa wa Italia ambaye alikua anakipiga katika klabu ya Juventus.

Fiorentina wamefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia baada ya kufikia makubaliano na klabu ya Juventus kwa ada ya uhamisho wa € Milioni 13 ambapo inaelezwa kufikia mpaka €18 Milioni kama nyongeza ya pesa hiyo kutokana na kiwango atakachooonesha ndani ya klabu hiyo.fiorentinaTaarifa zinaeleza kua klabu ya Fiorentina imefanikiwa kunasa saini ambayo wamekua walikua wanaihitaji kwelikweli, Hivo mpaka sasa klabu hiyo imeanza mchakato wa kukiimarisa kikosi cha timu hiyo kuelekea msimu ujao wa ligi kuu ya Italia na michuano mingine watakayokua wanashiriki.

Moise Kean anjiunga na klabu ya Fiorentina baada ya kushindwa kuonesha makali ndani ya kikosi cha Juventus lakini mchezaji huyo anaonekana anaweza kua msaada mkubwa ndani ya klabu yake hiyo mpya, Kwani wachezaji kadhaa wamewahi kutoka klabu moja na kushindwa kufanya vizuri lakini wakaenda kufanya vizuri klabu nyingine.

Acha ujumbe