Genoa Yamteua Patrick Vieira Kama Kocha Wao Mkuu

Vyombo vingi vya habari nchini Italia vinaripoti kwamba Genoa wameamua kumfukuza kazi kocha mkuu Alberto Gilardino na nafasi yake kuchukuliwa na nahodha wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira.

Genoa Yamteua Patrick Vieira Kama Kocha Wao Mkuu

Kulingana na Sky Sport Italia na mtaalam wa uhamisho Matteo Moretto, Genoa wameamua kuachana na Gilardino, ingawa uthibitisho rasmi kutoka kwa klabu bado haujachapishwa.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Genoa kwa sasa inashikilia pointi moja na nafasi moja juu ya eneo la kushushwa daraja la Serie A ikiwa na pointi 10 pekee kutoka kwa mechi 12 za mwanzo za msimu huu. Venezia na Monza, katika nafasi ya 19 na 20, wako pointi mbili pekee nyuma ya Grifone.

Genoa Yamteua Patrick Vieira Kama Kocha Wao Mkuu

Ripoti za leo zinaonyesha kuwa Vieira atakuwa mrithi wa Gilardono. Mshindi huyo wa fainali ya Kombe la Dunia 2006 amekuwa katika safari ya ukocha tangu alipostaafu mwaka 2011, akianza safari yake na timu za vijana za Manchester City, kabla ya kusonga mbele kupitia New York City FC, OSG Nice, Crystal Palace na Strasbourg.

Vieira pia anafahamiana vyema na mchezaji wa kiwango cha juu wa Genoa, Mario Balotelli, kutokana na mwaka waliokaa pamoja Manchester City mnamo 2010-11.

Acha ujumbe