Inter Milan Wamfungia Kazi Scamacca

Klabu ya Inter Milan imemfungia kazi mshambuliaji wa klabu ya West Ham Gianluca Scamacca ambaye amekua hapati nafasi ndani kikosi cha mabingwa hao Conference League.

Inter Milan wana mpango wa kutuma kiasi cha Euro milioni 20 kwa klabu ya West Ham ambapo ofa hiyo itakua na nyongeza vilevile hivo kutokana na ofa hiyo wanafainali hao wa ulaya wanaamini ofa yao itakubaliwa na West Ham na kuweza kukamilisha dili hili.Inter milanTaarifa zinaeleza kua Scamacca ameshakubali kujiunga na Nezzazuri msimu ujao, Lakini kkinachosubiriwa ni ofa mezani ambayo itaweza kuishawishi klabnu ya West Ham kumuachia mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia.

Inter Milan wanataka Scamacca akashirikiane na Lautaro Martinez pamoja na Eden Dzeko kwani mshambuliaji Romelu Lukaku hayupo kwenye mipango ya klabu hiyo kuelekea msimu ujao na atarudi kwenye klabu yake ya Chelsea.Inter milanMshambuliaji Gianluca Scamacca amekua hapati nafasi ndani ya kikosi cha West Ham kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo yamekua yakimuandama, Huku yeye akiamini anaweza kurudisha wake akirejea nchini Italia.

 

Acha ujumbe