Mkurugenzi wa klabu ya Inter Milan Ausilio amesema kua hawana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Armando Broja kwakua wanavutiwa na washambuliaji walionao klabuni hapo.

Ausilio ameweka wazi washambuliaji waliopo ndani ya klabu ya Inter Milan wanawatosha kutokana na ubora waliokua nao, Hivo klabu hiyo haitaingia sokoni mwezi Januari kutafuta mshambuliaji wa katikati.inter milanAusilio amesema wanajua kuhusu Broja amerudi uwanjani hivo karibuni na amefanikiwa kufunga, Lakini Mkurugenzi huyo ameweka wazi haoni nafasi ya mshambuliaji huyo kujiunga na klabu hiyo katika dirisha la usajili mwezi Januari.

Wanafainali hao wa ligi ya mabingwa ulaya msimu uliomalizika waliondokewa na mshambuliaji wao ambaye alikua kwa mkopo klabuni hapo Romelu Lukaku, Taarifa zikaeleza walikua wanamuwinda mshambuliaji huyo wa klabu ya Chelsea lakini mkurugenzi wa klabu hiyo amekanusha taarifa hizo.inter milanKlabu ya Inter Milan chini ya mkurugenzi wao Ausilio wameonesha kua washambuliaji wao waliopo klabuni hapo wanawapa kiburi ambao ni Lautaro Martinez, Marcus Thuram, Mark Arnautovic, na Alexis Sanchez na ndio maana wampiga chini mpango wa kumsajili Armando Broja.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa