Beki wa Manchester United, Harry Maguire, ameibuka katika orodha ya wachezaji wanaofuatiliwa na Inter Milan kuelekea dirisha la usajili la majira ya kiangazi, huku miamba hiyo ya Italia ikitafuta njia ya kuimarisha safu yao ya ulinzi kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Italia, Maguire ametolewa kwa mabingwa hao wa Serie A kupitia mawakala wake, jambo lililoifanya Inter kuanza kutathmini uwezekano wa kumsajili pamoja na chaguo nyingine zinazopatikana sokoni.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Harry Maguire ameibuka kwenye rada za Inter Milan, ingawa klabu hiyo bado inaendelea kuchunguza mbadala mbalimbali wa kuimarisha safu ya ulinzi,” zimeeleza taarifa hizo.
Inter wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika eneo la ulinzi kutokana na uwezekano wa kuondoka kwa baadhi ya mabeki wao wenye uzoefu. Francesco Acerbi na Matteo Darmian wanatarajiwa kuondoka mwishoni mwa mikataba yao, huku mustakabali wa Stefan de Vrij ukiendelea kuwa wa mashaka na Yann Bisseck akihusishwa na uhamisho wa kwenda Bayern Munich.
Hata hivyo, “Maguire bado si kipaumbele cha kwanza kwa Inter kwa sasa, kwani Nerazzurri wameelekeza nguvu zao katika harakati za kumsajili Oumar Solet kutoka Udinese kabla ya kuangalia chaguo nyingine.” Beki huyo wa England mwenye umri wa miaka 33 bado ana mkataba na Manchester United hadi mwaka 2027, lakini tetesi za kuondoka Old Trafford zinaendelea kushika kasi.


