Ripoti zinazoendelea kubamba nchini Uholanzi ni kwamba mkurugenzi wa PSV John de Jong ndiye mgombea wa hivi karibuni wa nafasi ya Ukurugenzi ya Roma.

Roma bado hawana mkurugenzi wa michezo baada ya kumtimua Gianluca Petrachi mnamo Juni, kwa hivyo Mkurugenzi Mtendaji Guido Fienga amekuwa akisimamia mazungumzo ya uhamisho.

Wakati mchakato wa kumsaka mrithi wa Petrachi ukiendelea, kumekuwa na majina mengi yaliyotajwa kama wagombea, pamoja na mkuu wa Lille Luis Campos.

John de jong
John de jong

Sasa kwa mujibu wa Voetbal International na Eindhovens Dagblad wanadai kuwa Roma wanaonyesha wazi kupendezwa kwa dhati na mkurugenzi wa PSV Eindhoven de Jong.

Hali yake huko PSV kwa sasa ni hali ya wasiwasi kidogo, kwani alikaribia kuondoka mara kadhaa tangu kuchukua kibarua hicho mnamo mwaka 2018 na alikasirisha mashabiki wa nyumbani kwa kumtimua Mark van Bommel mnamo mwezi Disemba.

Roma iko chini ya umiliki mpya msimu huu, tangia Dan Friedkin alinunua kutoka kwa James Pallotta mnamo mwezi Septemba.


 

 

UMEJARIBU HII POKER YA VIDEO?

Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

INGIA MCHEZONI!

23 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa